Bernard Arnault, mwanzilishi, na Mkurugenzi Mtendaji wa chapa ya kimataifa ya bidhaa za LVMH (Louis Vitton) amempita Elon Musk kama tajiri namba 1 duniani, Ukiangalia thamani ya hivi karibuni kulingana na Forbes.
Kwa mujibu wa Forbes, thamani ya Arnault na familia yake imeongezeka hadi dola bilioni 207.8 sawa na Tzs trilioni 530.9 baada ya ongezeko la dola bilioni 23.6, Tzs trilioni 60.3 siku ya Ijumaa, na kupita dola bilioni 204.5, Tzs trilioni 522.4 za Musk.
Orodha kwa sasa ipo hivi:
Watu 10 Matajiri zaidi duniani (Kwa Mujibu wa Forbes):
1. Bernard Arnault na familia $207.6 bilioni -Ufaransa
2. Elon Musk $204.7 bilioni -Marekani
3. Jeff Bezos $181.3 bilioni -Marekani
4. Larry Ellison $142.2 bilioni Marekani
5. Mark Zuckerberg $139.1 bilioni -Marekani
6. Warren Buffett dola bilioni 127.2 -Marekani
7. Larry Page $127.1 bilioni -Marekani
8. Bill Gates dola bilioni 122.9 za Marekani
9. Sergey Brin dola bilioni 121.7 za Marekani
10. Steve Ballmer $118,8 bilioni -Marekani
Cc;Forbes
#KonceptTvUpdates