Kufuatia Mvua zilizonyesha kwa Wingi Mkoani Dar es Salaam na Kufanya Uharibifu mkubwa katika baadhi ya maeneo hasa miundombinu, Askofu Josephat Gwajima kupitia Jimbo la Kawe aihoji Serikali juu ya hatma katika kutatua adha ya kukatikakatika kwa barabara ya jimbo hilo.
“Barabara za jimbo la Kawe zote zimevunjika na kukatika vipande vipande kwa sababu ya wingi wa mvua zinazonyesha, nimefika TARURA mkoa na wilaya wakasema hawana fedha, nini mpango wa dharura wa serikali kuokoa barabara hizo,” – Askofu Josephat Gwajima
JIBU: “Fedha za dharura tayari zimeanza kwenda kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini, pale jimboni kwa Askofu Gwajima tayari kuna milioni 598 ambayo imepelekwa katika eneo lake kuhakikisha barabara zinafunguliwa na kuanza kupitika,” – Naibu Waziri Deo Ndejembi
#KonceptTvUpdates