Mshambuliaji Simon Msuva amejiunga na klabu mpya Al najmah FC inayoshiriki Ligi ya nchini Saudi Arabia.
Msuva amejiunga na klabu hio akiwa mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba na klabu ya JS Kabylie ya Algeria.
Kutokana na ubora wake na kiwango kizuri alichoweza kukionyesha katika Michuano ya AFCON 2023 akiwa na timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” vimempa nafasi ya kusaini dili hilo jipya hivi karibuni.