Timu ya Taifa ya Congo DR yatolewa Michuano ya AFCON 2023 kufuatia kuruhusu goli 1 mnamo Dakika ya 65′ dhidi ya Wenyeji wa Michuano hiyo Ivory Coast ambalo lililosalia hadi dakika za mwisho za mchezo.
DR Congo imetolewa katika hatua ya Nusu Fainali ikiwa inawania tiketi ya kufuzu hatua ya Fainali kwenye Michuano hiyo.
Nyota wa Ivory Coast, Haller mnamo Dakika ya 65′ ndipo aliiadhibu Congo DR kwa kosa dogo lililofanywa kwenye Safu ya Ulinzi kwa kumuachia nafasi karibu na Goli.#KonceptTvUpdates