Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema kwa Mwaka 2024 Shirika la Fedha la Duniani (IMF) limesema kuwa Tanzania inatarajiwa kuwa kati ya nchi 20 zenye uchumi unaokuwa kwa kasi duniani.
Rais Samia amesema hiyo ni fursa kwa wawekezaji wa Norway chini Tanzania kwani pia ina mazingira mazuri ya kisiasa, kijiografia na kiuchumi.
Wakati akihutubia Mkutano wa Jukwaa la Biashara kati ya nchi hizo mbili, uliofanyika jijini Olso, Rais Samia amebainisha zipo kampuni kadhaa za Norway zilizotumia fursa hiyo vizuri kwa uchumi wa Tanzania.
Aidha, Samia amesema Kisiasa Tanzania ina amani nchi ya demokrasia imara wa mfumo wa vyama vingi wenye tunu za kuzingatia utawala bora, kuheshimu haki za binadamu na utawala wa sheria.
Kwa upande wa Kijiografia, Rais Samia amesema Tanzania inafaa kwa uwekezaji kwani ina Bandari ya Dar es Salaam katika Bahari ya Hindi, inayohudumia mataifa manne ya Afrika ianyopakana nayo.
Kiuchumi Tanzania ina Sera nzuri na imara za kiuchumi na kifedha huku ukuajiwa Pato la Taifa ukirejea kwenye 5.2% kwa mwaka. Unatarajiwa kufikia zaidi ya 6% kwa mwaka ujao kama ilivyokuwa kabla ya COVID 19.
Rais Samia amesisitiza fursa tano za kipaumbele zikiwemo uwekezaji katika nishati mbadala, kilimo, mafuta na gesi, mifuko ya uwekezaji, miundombinu na usafirishaji.
Rais Samia ameanza ziara ya kitaifa nchini Norway kwa muda siku mbili baada ya kutoka takita ziara ya Kihistoria huko Vatican ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Francis.
Cc; Ikulu Mawasiliano
#KonceptTvUpdates