Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amewataka Wambunge kuacha kuendelea kuuliza masuala yanayohusiana na Vyoo bungeni kufuajia Wizara husika ilishawahi kutolea ufafanuzi tayari, hivyo kwa hapa nchi ilipofikia haipendezi kuendelea kurudia rudia mada moja ili hali ilishatolewa ufumbuzi.
“Wabunge hapa wameuliza kuhusu vyoo na wewe (Naibu Waziri Dugange) kwenye majibu yako ukatoa majibu, nafikiri kwa nchi yetu tulipofikia ni mahali ambapo hatutakiwi kuwa tunazungumza vyoo kwenye zahanati, choo kimoja pale vyoo viwili pale, serikali inafanya kazi sana na hakuna sababu ya kujadili vyoo humu ndani,” – Spika wa Bunge, Dkt @TuliaAckson
#KonceptTvUpdates