Mtendaji Mkuu wa Young Africans Sports Club, Andre Mtine [Kulia], akipokeza Tuzo Maalum ya ‘Humanitarian Awards’ kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Professor Jay Foundation, Florian Rutabigwa.
Young Africans Sports Club ilipata tuzo hio kwenye hafla iliyofanyika jana mchana , katika hospitali ya taifa, Muhimbili, kutokana na mchango wa Klabu hiyo katika kufanikisha programu maalum ya figo inayoendeshwa na taasisi hiyo.