Jeshi nchini Guinea, ambalo lilichukua mamlaka zaidi ya miaka miwili iliyopita, limeivunja serikali ya mpito katika taifa hilo la Afrika Magharibi na kusema kuwa litateua utawala mpya.
Jeshi linasema litateua serikali mpya, lakini halijaonyesha ni lini hiyo itakuwa.
Viongozi wa kijeshi walitoa taarifa ya video Jumatatu kusema kwamba wakurugenzi wa baraza la mawaziri, katibu mkuu na manaibu wao watasimamia hadi serikali mpya iundwe.
Bado haijafahamika ni vipi uvunjifu huo, ambao Katibu mkuu wa ofisi ya rais, Amara Camara hakutoa sababu mara moja juu ya nchi hiyo au viongozi wakuu wa serikali mpya wangekuwa nani.
Chini ya shinikizo la kimataifa, kiongozi wa kijeshi Kanali Mamady Doumbouya alikuwa ameahidi kurudisha mamlaka ya serikali kwa raia waliochaguliwa ifikapo mwisho wa 2024.
Cc;Aljazeera
#KonceptTvUpdates