Wanasarakasi kutoka Tanzania, Fadhili Ramadhani na Ibrahim Jobu, wanaounda kundi la “Ramadhani Brothers” wameibuka washindi wa “AGT: Fantasy League” usiku wa kuamkia Jumanne na kuondoka na Dola za Marekani 250,000 (Takriban Tsh. Milioni 637.5)
Kundi hilo limeweza kuwashinda washiriki wengine bora kama vile The Pack Drumline, V.Unbeatable, Sainted na Musa Motha.
Ramadhani Brothers wanakuwa Watanzania wa kwanza kufanikiwa kushinda Mashindano ya “AGT”. Wakizungumza baada ya kutangazwa Washindi, wamesema Fedha hizo wataziwekeza katika Vifaa vya Mazoezi Nchini
#KonceptTvUpdates