Kupitia Jukwaa la Kodi na Uwekezaji 2024, Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Philip Mpango ameeleza kuwa Mapato ya Serikali yameongezeka hadi kupelekea Serikali kuongeza Bajeti kwa Mwaka 2023/2024
“Makusanyo ya Mapato ya Serikali kwa Kipindi cha miaka mitatu iliyopita yameongezeka kutoka Shillings trilioni 17.6 Mwaka 2021 hadi Shillingi trilioni 22.6 Mwaka 2022/23. Ongezeko hilo la ukusanyaji wa Mapato imewezesha Serikali kuendelea kuongeza bajeti kutoka shilingi trilioni 36 Mwaka 2021/22 hadi Shilingi trilioni 44.4 mwaka 2023/24” Mhe. Dkt. Philip Mpango -Makamu wa Rais Tanzania
#JukwaalaKodinaUwekezaji
#KonceptTvUpdates