Mahakama ya Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma Februari 27, 2024 imemuhukumu kifungo cha Miaka Therathini (30) jela Goodluck Ignas Ndunguru (21), Fundi Kushino, Mkazi na Kijiji cha Mateka Wilaya ya Mbinga baada ya kupatikana na hatia kwa kosa Kubaka.
Akisoma hukumu hiyo ya kesi ya Jinai Na. 648 ya mwaka 2024, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Mhe. Haule alisema Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pasipo kuacha shaka yoyote.
Mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Desemba 21,2023 na kufikishwa mahakamani Januari 09, 2024 ambapo Februari 27,2024 hukumu ilitoka na kupatikana na hatia ya Makosa hayo.
See translation