Mkaguzi wa magari wilaya ya Masasi mkoani Mtwara ,Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Stephen Changanga leo akiwa pamoja na watendaji wengine wa Usalama Barabarani wakifanya ukaguzi wa magari yanayosafirisha abiria kwenye maeneo mbalimbali katika stendi ya mabadi masasi mkoani Mtwara.
Katika ukaguzi huo magari yalikaguliwa ,Ratiba,Vibali,Leseni ya Safari kutoka LATRA,mifumo ya Taa zinazoongezwa kwenye magari hayo sambamba na wale walioweka vimulimuli bila ya kuwa na kibalimaalum.
Pia magari hayo yalikaguliwa ubandikaji wa stika angavu maarufu kama 3D kwenye namba za magari
Cc;Jeshi la Polisi
#KonceptTvUpdates