Watuhumiwa 79 wamekamatwa kwa tuhuma za makosa mbalimbali wakiwemo watatu waliojifanya Maofisa wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuwanyang’anya wananchi fedha zao.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini Kwake Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. RASHID HADID RASHID amesema watu hao ambao hakuwataja majina kwasababu za upelelezi wamekamatwa kufuatia Opereshen za pamoja zinazoendelea kufanywa katika Mkoa huo.
Amefahamisha kuwa, watu wengine watatu wamekamatwa kuhusika na makosa ya udhalilishaji, wawili wanatuhumiwa kupatikana na dawa za kulevya na 67 Makosa ya kuwabughudhi watalii.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP DANIEL SHILLAH amesema Jeshi la Polisi Mkoani humo limejipanga kuimarisha ulinzi Maeneo ya kitalii na maeneo mengine na amewataka Mapapasi (beach boys) kufuata taratibu za kutoa huduma kwa watalii.
#KonceptTvUpdates