Umoja wa Afrika Mashariki (EAC), umekanusha uvumi unaosambaa mitandaoni kuwa umezindua Matumizi ya Sarafu moja kwa Wanachama wake na kueleza kuwa bado suala hilo lipo kwenye mchakato.“Sekretarieti ya EAC inapenda kuwafahamisha wadau wetu wote kwamba safari ya Nchi Wanachama katika kutumia sarafu moja bado ni kazi inaendelea. Tafadhali puuza uvumi wowote unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuzindua noti mpya za eneo hili.” Taarifa kutoka EAC
Aidha kupitia mtandao “X” Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. January Makamba amesisitiza hilo kwa kuandika.. “Hizi taarifa si za kweli. Taratibu na vigezo vya kiuchumi na kitaasisi vya kufikiwa kwa Umoja wa Fedha (Monetary Union)/Sarafu Moja (Single Currency) kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki bado kukamilika. Mapendekezo ni kufika hatua hiyo mwaka 2031. Ukurasa rasmi wa Jumuiya ni @jumuiya”
#KonceptTvUpdates