Akithibitisha kushikiliwa kwa mtuhumiwa huyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi SACP Kaster Ngonyani amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa Machi 4, 2024 baada ya msako unaoendelea wa kuwabaini na kuwakamata watuhumiwa wanaohujumu mamlaka ya maji kwa kung’oa koki ambazo watumiaji wa maji wanakuwa wameunganishiwa majumbani na kwenda kuziuza kama chuma chakavu.
Nae Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo Bi. Rehema Nelsoni amelishukuru Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kwa kuweza kumkamata mtuhumiwa na amebainisha kuwa wahalifu hao pindi wanapong’oa koki hizo mamlaka imekuwa ikipata hasara kwa upotevu mkubwa wa maji na ameongeza kuwa koki zilizokamatwa zina jumla ya thamani fedha za Kitanzania shilingi milioni 4.5
Kamanda Ngonyani amesema mtuhumiwa bado anaendelea kuhojiwa lengo kupata mtandao wote wa wahalifu hao na mara baada ya taratibu zote za upelelezi kukamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.