‘Dawa za kulevya zilinipoteza, mke wangu akanisaidia kubadilika’ – Mr. Blue
Mwanamuziki wa kizazi kipya ‘Bongo flava’ Herry Sameer Rajab almaarufu kama Mr. Blue ameongea kuhusiana na safari yake ya muziki na maisha yake kwa ujumla, huku akikiri kwamba kuna kipindi alipotea kwenye müziki kutokana na kufuata starehe na marafiki wabaya.
–
Nguvu ya familia hasa mke na watoto ndivyo vilivyompa nguvu ya kurudi katika ramani ya muziki na kufanya vizuri hasa kwasababu aliingia katika majukumu ya kifamilia.
–
Mr Blue ameleza hilo bayana alipofanya mahojiano na mtangazaji kinara wa BBC @roncliffeodit katika studio mpya za kurusha matangazo kidigitali za BBC zinazozindulia Ijumaa hii jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Cc; Via BBC Swahili
#KonceptTvUpdates