Askari Wanawake wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha wameungana na Wanawake wengine wilayani humo kuunga Juhudi za Mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu za kuutangaza utalii kwa kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Arusha kwa lengo la kujionea vivutio vinavyopatikana katika hifadhi hiyo.
Aidha wamebainisha kuwa wameona fahari kutembelea hifadhi hiyo yenye vivutio mbalimbali ambapo wametoa wito kwa Watu wengine kuwa na utaratibu wa kwenda kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo hapa Nchini kwani pamoja na kuona uzuri uliopo lakini pia watajifunza mambo mengi.
#KonceptTvUpdates