Jeshi la Polisi mkoani Geita limepiga maarufu bodaboda kupakia Watoto juu ya mzigo ili iwe ni tahadhari kutohatarisha usalama wao kutokana na tukio la ajali mbaya linaloweza kujitokeza muda wowote bila ya kutarajia.
Marufuku hiyo imetolewa Machi 9,2024 na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (A/INSP) Phabian Welwel wa kikosi cha usalama barabarani alipokutana na mwendesha pikipiki (bodaboda) katika Kituo cha mabasi Geita akiwa amempakia mtoto juu ya gunia la mahindi jambo ambalo linahatarisha usalama wa mtoto huyo.