Shirikisho la Viwanda nchini (CTI), limeiomba serikali na taasisi zake kulinda viwanda vya ndani kwa kununua bidhaa zinazotengenezwa na viwanda hivyo kama njia ya kulinda hifadhi ya fedha za kigeni.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa shirikisho hilo, Leodegar Tenga, wakati ujumbe wa shirikisho hilo ulipotembelea kiwanda cha mabati, nondo na plastiki cha Lodhia Industries kilichoko Kisemvule Mkoa Pwani kujionea shughuli za uzalishaji kiwandani hapo.
#KonceptTvUpdates