Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake, Mheshimiwa Japhet Hasunga imetembelea na kukagua ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Wizara ya Nishati awamu ya II katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Akizungumza mara baada ya ukaguzi wa jengo hilo Mheshimiwa Hasunga amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felches Mramba kumsimamia Mkandarasi kwa ukaribu ili aweze kukamilisha ujenzi huo kwa muda waliokubaliana.
Aidha, Wajumbe wa Kamati PAC pia wametembelea na kukagua Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Wizara ya Afya katika Mji wa Serikali Mtumba.