Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amefanya mazungumzo na uongozi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) ukiongozwa na Naibu Mtendaji Mkuu wa wake Marie-Hélène Loison, Ufaransa AFD, ambapo mazungumzo hayo yamehusu uwekezaji na utekelezaji wa awamu ya pili ya Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira Ziwa Victoria katika jiji la Mwanza ili kumaliza uhaba wa maji katika jiji hilo.
Waziri Aweso katika mazungumzo hayo kwa upande wa Morogoro amewasilisha ombi la nyongeza ya uwekezaji wa fedha zitakazowezesha kuongeza ujenzi wa miundombinu ya usambazaji maji pamoja na ujenzi wa miundombinu ya majitaka ambapo SFD walitenga kiasi cha Euro milioni 70 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya majisafi pekee.
Pamoja na hayo amewasilisha rasmi kwa mara ya kwanza ombi la fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya kutoa maji katika ziwa Tanganyika kupeleka mikoa ya Katavi na Rukwa
Mhe Aweso amesema hatua hiyo ni mafanikio ya ajenda iliyobebwa na Wizara ya Maji katika ziara ya kikazi nchini Ufaransa na itafanikisha upatikanaji wa maji katika maeneo ambayo miradi ya ujenzi wa miundombinu imekamilika na inaendelea.
Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira Ziwa Victoria katika jiji la Mwanza, awamu ya kwanza ilitekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali, Benki ya Uwekezaji ya Ulaya na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD).
#KonceptTvUpdates