Na Mwandishi Wetu;
#HAMASA: Baa ya Dance Club iliyopo Mwenge Mpakani jijini Dar es Salaam, imezindua kampeni maalum kwa ajili ya kutoa fursa kwa mashabiki wa timu za Simba na Yanga kutoa hamasa kwa timu zao wakati wa michezo ya robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika (#CAFCL) na kueleka mpaka nusu fainali na fainali endapo zitafuzu.
Kampeni hiyo inayojulikana kama “MPAKA FAINALI INAWEZEKANA” Dance Tuvushe!, inalenga kutoa hamasa kwa wateja wa Dance Club ambao ni mashabiki wa Simba na Yanga kuhakikikisha wanahamasika katika kushangilia timu zao kufika fainali za Klabu bingwa Afrika.
“Lengo letu ni kuwafanya wateja wa Dance Club ambao ni mashabiki wa michezo hususani wa timu za Simba na Yanga kuwa katika mazingira mazuri na pia kuhakikisha wanafuatilia mpira moja kwa moja (live) katika screen kubwa na za kutosha Ndani ya Dance Club,” amesema Jaffary Lucas -Meneja Burudani wa Club hiyo.
Kwa mujibu wa Jaffary, wateja wa Dance Club ambao ni mashabiki wa Simba na Yanga na wapenzi wa mchezo wa soka kwa ujumla wataweza kununua kadi ambazo ni Green na Red card za Dance Club Sport Fans.
“Wateja wetu wataweza kutumia kadi hizo kuingia kuangali mpira na kushangilia timu zao bila kiingilio na kubugudhiwa, lengo likiwa ni kuongeza uzalendo kwa timu zetu haşa katika kipindi Hiki cha uwakilishi wa Taifa pasipo kujali ushabiki,”. alisema
#CAFChampionsLeague #Dar #MkapaStadium #HomeGames #AwayGames
#Win #DanceClubBar #SimbascVsAlahly #YangaVSMamelodi
#KonceptTvUpdates