Miongoni mwa Taarifa kubwa inayoshika vichwa vya habari kutokea Marekani zamuhusu mwanamuziki wa HipHop P Diddy kuvamiwa na Idara ya Usalama wa Taifa hilo nyumbani kwake Los Angeles na Miami.
Ndege binafsi ya Diddy, inayorushwa chini ya LoveAir LLC, imefuatiliwa hadi Antigua huku kukiwa na uvamizi wa Maafisa usalama katika nyumba zake nchini Marekani, ikiwa ni pamoja na Los Angeles na Miami, ambapo wanawe Justin na King waliripotiwa kuwekwa chini ya ulinzi.
Chanzo cha Usalama kuvamia nyumbani kwake ni uchunguzi wa madai ya kesi zinazomkabili za unyanyasaji wa kijinsia na biashara ya ngono.
Baada ya taarifa hizo Diddy alionekana uwanja wa Ndege wa Miami, na ndege yake binafsi kufuatiliwa mpaka visiwa vya Caribbean.
Taarifa rasmi kutoka kwa wawakilishi wa Diddy au timu ya wanasheria bado hazijatolewa kuhususiana masuala hayo.
#KonceptTvUpdates