Kampuni ya Mtandao wa Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania imezindua rasmi kifaa Cha Kisasa kinachojulikana kama (Airtel Smart Box) kinachomuwezwasha mteja wa Airtel kupata WiFi na Internet Kwa kasi ya masafa ya 5G akiwa maeneo mbalimbali nchini Tanzania, ikiwa ni kudhihirisha muendelezo wa uwekezaji mkubwa inayofanywa na Airtel katika kuboresha huduma za Internet nchini.
Kupitia teknolojia ya kasi ya 5G, wateja wataweza kupakua Kwa kasi zaidi Hadi 50 Gbps, kufanya ‘streaming’ na mikutano Kwa njia ya Mtandao bila kikomo na Kwa urahisi.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Timea Chogo amesema Airtel inajivunia kuendelea kuleta mabadiliko katika Utoaji huduma za Internet kupitia Airtel 5G, na kuchochea kuenea Kwa huduma hiyo ambayo ni matarajio ya watanzania wengi, katika kuwezesha watu binafsi na wafanyabiashara kutumia fursa ya huduma hiyo kukamilisha mahitaji yao kidigitali.
Kwa upande wake, Balozi wa Airtel Tanzania, Naseeb Abdul @diamondplatnumz teknolojia hiyo imemsaidia Kwa kiasi kikubwa Kwa matumizi ya nyumbani na katika kazi zake za Sanaa hususan kuupload nyimbo zake kwa kasi ya 5G na kufanya matangazo ya Mubashara kupitia Wasafi TV hususani kipindi cha Wasafi Festival.
#KonceptTvUpdates