·
Zikiwa na maboresho ya program za usalama na uono angavu zaidi, simu mpya za toleo la Galaxy A zinaleta uhuru wa matumizi ya simu kwa watu wo
Samsung Electronics Co., Ltd. leo imezindua Galaxy A55 5G na Galaxy A35 5G, matoleo mawili mahiri yanayoonyesha dhamira endelevu ya Samsung ya kuweka ubunifu bora zaidi wa simu za mkononi kwa matumizi ya kila mtu. Simu zote mbili zinakuja na programu nyingi za usalama kama vile Knox Vault, pamoja na uwezo mpya wa upigaji picha unaochochewa na ubunifu wa kamera wa hali ya juu wa Galaxy na kioo cha kisasa ambacho hubadilika kulingana na mazingira ya watumiaji kwa kutumia Vision Booster.
“Kwa mfululizo wa matoleo ya Galaxy A, tunapanua teknolojia yetu ya kisasa kuwafikia watu wengi zaidi ili wanufaike,” alisema Mtendaji Mkuu wa Samsung Electronics Tanzania, Manish Jangra. “Tunafurahi kufungua fursa zaidi kwenye aina ya Galaxy A mwaka huu, pamoja na kujumuisha program ya usalama ya Samsung Knox Vault kwa mara ya kwanza kwenye matoleo haya. Tunajivunia kuwawezesha watumiaji wa simu hizi kufurahia matumizi bora ya simu kwa usalama na wenye kutumainiwa.”
Burudani na Ubunifu wenye Upigaji picha kwa uhuru na Kioo cha kuvutia
Ikiwa imeboreshwa na Nightography, Galaxy A55 5G inapiga picha angavu na nzuri zaidi hata kwenye mwanga hafifu. Hii inamaanisha kwamba hata wakati wa usiku unaweza kupiga picha kwa uwezo wa hali ya juu. Uchakataji wa Mawimbi ya Picha ya AI (ISP) ya hali ya juu ya Galaxy A55 5G hutoa picha nzuri zenye mwanga hafifu ukilinganisha na matoleo ya nyuma ya Galaxy A. Sio tu mandhari ambayo yanaonekana vizuri. Mazingira ya upigaji picha za usiku na 12-bit HDR video huhakikisha watu katika kila picha wanaonekana vizuri ili kunasa kumbukumbu ukiwa na marafiki na familia bila kutegemea kuwa na mwanga wa kutosha.
Galaxy A55 5G na Galaxy A35 5G zote zina uwezo wa kipekee wa upigaji picha ambao Samsung Galaxy imekuwa ikisifika nao, hii ni pamoja na programu kama vile za uimara wa muonekano wa picha (OIS) na uimara wa picha za kidijiti za video (VDIS) ambazo huzifanya picha na video kuonekana vizuri hata ukirekodi mahali popote pale.
Simu hizi mpya pia zinaendeleza utamaduni wa matoleo ya Galaxy A wa kufanya matumizi ya simu za mkononi kufurahiwa na kufikiwa na watu wote. Watumiaji wanaweza kufurahia kutazama matamasha yanayoendelea au kuvinjari mitandao ya kijamii kwa kutumia kioo cha Super AMOLED, kikionyesha picha za kuvutia katika uangavu wa hali ya juu. Pia watarajie skrini ya inchi 6.6 kwenye Galaxy A55 5G na Galaxy A35 5G yenye mwonekano safi na angavu ikiwa nyepesi kutokana na uwepo wa Vision Booster.
Uhuru wa Ubunifu wa Samsung wa Usalama wenye Nguvu Zaidi ili Kulinda Wateja kwa Muda Mrefu zaidi
Galaxy A55 5G na Galaxy A35 5G zimekuja na program ya Samsung ya usalama yenye ubunifu zaidi kwenye aina ya Galaxy kwa watumiaji wa matoleo ya Galaxy A kwa mara ya kwanza: Samsung Knox Vault. Suluhisho la usalama linalokinzana na majaribio ya kiuhalifu, Samsung Knox Vault inatoa ulinzi wa kina dhidi ya mashambulizi ya kifaa na programu kwa kutengeneza mazingira salama ya utendaji kazi ambayo yametengwa mfumo na kihifadhi kumbukumbu. Inaweza kusaidia kulinda taarifa muhimu zaidi kwenye simu, ikiwemo taarifa za kufunga skrini, kama vile misimbo ya PIN, nywila na’pateni’. Pia hulinda taarifa muhimu za kuifunga simu, taarifa binafsi za watumiaji zilizohifadhiwa kwenye kifaa. Ni mtumiaji aliye na kitambulisho sahihi cha skrini iliyofungwa pekee ndiye anayeweza kupata taarifa zake, hata kama kifaa kikipotea au kuibiwa.
Galaxy A55 5G na Galaxy A35 5G pia zinalindwa na Samsung Knox, program yenye matobaka tofauti ya kiusalama ya Galaxy. Samsung Knox, mojawapo ya programu ya usalama inayoaminika zaidi ulimwenguni, imetengenezwa kulinda taarifa muhimu na dhidi ya madhaifu kwa kutumia njia salama za kudumu katika simu, utambuzi wa matishio wa muda halisi na ulinzi shirikishi, ikichukua mbinu kikamili katika mfumo mzima wa ikolojia wa Galaxy.
Njia zaidi za kuendelea kuwa salama, matoleo ya Galaxy A ina ‘Auto Blocker’, program jumuishi iliyo ndani ya kifaa kwa usalama wa ziada. Inapowashwa, inaweza kuzuia uwekaji wa programu kutoka kwa vyanzo visivyoidhinishwa, kukagua usalama wa programu ili kugundua zisizofaa na kuzuia uwekaji wa programu zinazoweza kuleta athari kwenye kifaa chako kikiwa kimeunganishwa kwa waya wa USB. Watumiaji wapya pia wataweza kufikia ‘Dashibodi ya Usalama na Faragha’ ya Galaxy, hivyo kurahisisha kuona na kudhibiti kinachoendelea kwenye taarifa zao na kutoruhusu chochote wakati wowote wanaoamua. Pia watafurahia kuwa sehemu ya program ya kulinda taarifa zao, ambayo huwezesha ushiriki salama na uliofungwa kwa siri kwa kutumia mafaili ya faragha yenye taarifa muhimu binafsi au za kifedha. Kuhakikisha usiri, watumiaji wanaweza kudhibiti ruhusa za ufikiaji kwa mpokeaji na tarehe ya mwisho wa matumizi ya faili, huku pia wakichagua kuzuia upigaji picha wa skrini (screenshot) au upakuaji.
Simu mpya za toleo la Galaxy A zinaonyesha kujizitati kwa Samsung kuhakikisha kuwa vifaa vya Galaxy vinaendelea kuwa salama na kuboreshwa kwa muda mrefu zaidi. Kwa kutumia Galaxy A55 5G na Galaxy A35 5G, watumiaji wataendelea kunufaika mpaka toleo la kizazi cha nne cha uboreshaji wa Android OS na One UI na miaka mitano ya maboresho ya kiusalama, kuboresha mzunguko wa maisha wa simu kwa kuziweka zikiwa na matoleo mapya zaidi ya Galaxy na program za Android.
Kuunganishwa kwa Urahisi na Mfumo Mpana wa Ikolojia wa Samsung Galaxy
Galaxy A55 5G na Galaxy A35 5G zinaendana kikamilifu na mfumo wa ikolojia wa Galaxy ukiwapatia watumiaji urahisi na mifumo ya matumizi iliyojumuishwa katika vifaa vya Galaxy. Watumiaji wanaweza kufuatilia maendeleo yao ya kiafya kwa kujiungana na Galaxy Fit3 au Galaxy Watch6 kwenye matoleo mpaya ya simu za Galaxy A. Shukran kwa ‘Auto Switch’, simu zinazoingia zitaunganishwa moja kwa moja kwenye Galaxy Buds FE kwa urahisi zaidi.
Kupata taarifa zaidi kuhusu Samsung Galaxy A55 5G, Galaxy A35 5G na matoleo mengine ya simu za Galaxy, tafadhali tembelea: Samsung Newsroom, Samsung Mobile Press na Samsung.com.
-MWISHO-