Mgombea Urais wa Chama cha FPR nchini Rwanda, Paul Kagame ameshinda tena kiti hicho baada ya kupata kura 7,099,810 sawa na asilimia 99.15 ya kura zote zilizopigwa ni milioni 9,071,157.
Kagame amewashinda Frank Habineza wa Chama cha Democratic Green aliyepata jumla ya kura 38,301 sawa na asilimia 0.53 na Phillipe Mpayimana aliyepata kura 22,753 sawa na asilimia 0.32.
Wananchi wa Rwanda jana Jumatatu, Julai 15, 2024, walipiga kura katika Uchaguzi Mkuu ikiwa ni mara ya nne tangu yatokee mauaji ya kimbari mwaka 1994.
#KonceptTvUpdates