Zifutazo ni dondoo nne za kuzingatia ukiwa umeachwa na mpenzi wako
1. Jifunze kusamehe najua kuachwa kunaumiza sana kwa mtu aliye wahi kuachwa anaweza akawa shuhuda mzuri wa hili. Msamaha ni lazima hata kama mtu alikukosea vipi msamaha wa kweli huondoa uchungu na huzuni endapo ukaendelea kumuona huyu aliyekuacha.
2.Kubali kuwa wa tofauti sasa. Kinachowashinda watu ni kushindwa kupata mpango wa pili baada ya kuachwa. Unapoachwa jifunze kujitengenezea maisha yako jipende. , soma vitabu,vaa vizuri pendeza kabisa hata unaweza kujitoa out na ikiwezekana fanya mambo ambayo hujawahi kuyafanya kabisa katika maisha yako itakuletea furaha kipindi cha upweke kuliko kukimbilia kimbilia kwenye mahusiano mengine tena mbaya zaidi yasiyo na afya, hii itakupunguzia msongo wa mawazo na hasira. Kufanya vitu vipya vinasadia katika kutengenezea hatua mpya.
3. Kkuachwa sio mwisho wa maisha, ukichwa amini safari mpya inanza hivi karibuni. Ukishindwa kusamehe utashindwa kufungua moyo kwa safari nyingine.
4. Tafuta ushauri kwa watu upate msaada wa kimawazo namna ya kuondokana na hasira au huzuni endapo utakumbana nazo. Tafuta watu wachache wakuwashirikisha mambo yako zingatia sio kila kitu ni chakumweleza mtu.