#UCHUMI Serikali ya Ethiopia imekubali sarafu yake kuuzwa katika soko huria badala ya kiwango kilichowekwa kama sehemu ya mageuzi yaliyolenga kupata mikopo kutoka kwa wakopeshaji wa kimataifa ili kuimarisha uchumi wake.
Thamani ya birr dhidi ya dola ilishuka kwa asilimia 30% baada ya kuruhusiwa kuelekea Jumatatu, ilithibitisha benki kubwa zaidi nchini humo, Commercial Bank of Ethiopia.
Kuondolewa kwa kiwango kilichowekwa na benki kuu ni sehemu ya mageuzi makubwa yanayolenga kupunguza upungufu sugu wa fedha za kigeni uliouathiri uchumi wake.
Nchi ya hiyo ya Afrika inatumaini mabadiliko haya yataiwezesha kupata mikopo kutoka kwa wakopeshaji kama Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia. Imekuwa katika mazungumzo na IMF kuanzisha mpango mpya wa mikopo.
Ethiopia ilikua nchi ya tatu ya Afrika katika miaka mitatu iliyopita kushindwa kulipa deni lake la serikali mwishoni mwa mwaka 2023.
Hali hiyo ilichangia kushushwa kwa kiwango chake cha mikopo hadi “eneo la taka” na shirika la ukadiriaji la Fitch mwaka jana.
#KonceptTvUpdates