Wanasayansi na wahifadhi wa mazingira, leo, siku ya Ulinzi wa Tembo/Ndovu Ulimwenguni, wameikabidhi serikali ya Tanzania arafa la ombi la kimataifa la sahihi zaidi ya 500,000 inayonuiwa kuwarai kutamatisha uwindaji wa ndovu katika maeneo yake yanayopakana na Kenya.
Hii ni kutokana na hatua ya utawala wa Tanzania kutoa vibali vya uwindaji wa ndovu wenye pembe kubwa zaidi almaarufu Super Tuskers katika hifadhi ya wanyama ya Amboseli- West Kilimanjaro. Watano kati ya ndovu hao walisakwa na kuuliwa na wawindaji wa nyara kaskazini mwa nchi ya Tanzania katika muda wa miezi minane iliyopita. Vibali zaidi vyatarajiwa kupokezwa hivi karibuni.
Muungano wa wahifadhi wa ndovu wametuma maombi yao kupitia jumbe kwa ubalozi wa Tanzania, Nairobi na Ikulu ya Tanzania katika taarifa kwa wanahabari katika hoteli moja ya Nairobi.
Japo inatambuliwa kuwa swala la usimamizi wa ndovu ni jukumu la serikali ya Tanzania, wanasayansi walikumbusha viongozi hawa wawili kuwa jamii hii ya ndovu ni rasilmali asili ya nchi zote mbili kwa hivyo ulinzi na uhifadhi wao unawezeshwa tu kwa mustakabali wa pande zote mbili.
“Maangamizi ya hawa ndovu si pigo linaloelekea tu kupunguza idadi yao bali ni pigo kwa juhudi zetu katika shughuli za uhifadhi,” alisema Dkt. Cynthia Moss, mwanzilishi wa Amboseli Trust for Elephants.
Ombi hili lanuia kusisitiza umuhimu wa kiikolojia na kiuchumi wa ndovu waliomo katika maeneo ya Amboseli- Kilimanjaro Magharibi (West Kilimanjaro). Eneo hili husheheni chemichemi muhimu ya kijenetiki inayozingira mipaka ya mataifa haya mawili.
Kufikia mwaka wa 2023, palikuwa na muda wa miaka 30 bila visa vya uwindaji wa ndovu kuripotiwa. Visa vya matukio ya uwindaji vya hivi karibuni vimechangiwa na kwota ya vibali ya mwaka 2022 vilivyotolewa kwa Kilombero North Safaris. Mara ya mwisho tukio la kuhuzunisha la uwindaji wa Super Tuskers ilitokea mwaka wa 1994.
Hii ilipeleka walimwengu kutoa vilio vikali wakati ndovu wanne mashuhuri (RBG, Sleepy, Sabulu na Oloitipitip), waliokuwa wakitumiwa katika utafiti na mradi wa Amboseli Elephant Reseach Project, walipigwa risasi na kuuliwa na wawindaji wa nyara katka eneo la Tanzania. Kutokana na vilio vya umma, makataa ya uwindaji wa nyara kwa ndovu hawa wanaovuka mpakani yalitolewa na nchi zote mbili mwaka wa
1995.
Vibali vipya vya uwindaji vinatishia maangamizi ya tembo hawa wenye thamani kubwa. Ndovu 10 pekee wenye pembe za zaidi ya kilogramu 45 (100 lbs) kwa kila pembe wamesalia katika mfumo-ikolojia ya Amboseli ambayo ina idadi kubwa zaidi ya wanyama hawa katika sehemu moja.
Uwindaji utawafanya wanyama hawa kutoweka kufikia miaka mitatu zijazo. “Mauaji ya hivi karibuni ya Super Tuskers inatuhusu sana tukizingatia idadi yao ndogo na mchango mahususi ya hasa ndovu dume katika jamii ya tembo,” alisisitiza
Dkt. Joyce Pool, mkurugenzi wa shirika la Elephant Voices. Ingawa Kenya iliharamisha uwindaji mwaka wa 1977, hatua inayoendelea kutimizwa, bado ni halali katika nchi ya Tanzania ambako makampuni ya biashara ya uwindaji
wa nyarahupokezwa leseni kwa niaba ya wateja wao.
Rai ya wadau wa kimataifa katika ukumbi wa tovuti wa Avaaz iliungwa mkono na muungano wa mashirika zaidi ya 50 yanayoshughulikia uhifadhi wa ndovu barani Afrika. Wadau hawa waliiomba utawala wa Tanzania kushirikiana na wenzao wa
Kenya ili kulinda urithi huu wa kiasili. Dkt. Paul Kahumbu, mkurugenzi mtendaji wa shirika la WildlifeDirect alisema, “Tunawahimiza rais Ruto wa Kenya na rais Samia Suluhu wa Tanzania wakutane na kuweka makubaliano/mkataba kuhusu umuhimu wa kuhifadhi rasilmali hii ambayo ni tunu kwa sayansi na uchumi, ni miliki ya nchi zote mbili na faida zake hupiku mapato ya haraka ya uwindaji wa nyara katika nchi moja.”
Ombi hili pia laangazia njia hasi na zisizo za kimaadili za uwindaji, zikiwemo
matumizi ya ndege za helikopta kuwasaka ndovu na uchomaji au kuzikwa kwa
mizoga ili kuficha ushahidi.
Dkt. Winnie Kirui wa shirika la Elephant Protection Innitiative na shirika la utafiti la Mpala Research aliongezea akisema, “Mauaji ya ndovu hawa kama spoti ni jambo linalokera na la mtazamo finyu ambalo halistahimiliki kiuchumi.”
Kuhusu Amboseli Super Tuskers
Eneo zima la Amboseli- West Kilimanjaro linajumuisha karibu wanyama 2000 ambao mazingira yao ni eneo zima la mpaka wa Kenya na Tanzania. Karibu 600 ni ndume ambao kwao, 10 ni Super Tuskers. Inajumuisha ndovu dume wakomavu walio na pembe kubwa zaidi barani Afrika kwa mujibu wa umbile/ umbo-jeni zenye upekeewalio nao, (Pembe kubwa zaidi kupatikana, kuhifadhiwa na kuonyeshwa katika makavazi ya British Museum zatoka kwa jamii hii ya ndovu) pamoja na juhudi za miaka mingi za ulinzi dhidi ya uwindaji wa nyara na uwindaji haramu.
Kwa maelezo/ habari zaidi
Wasiliana na: muthoni@wildlifedirect.org au piga +254 746 327 244