#KIMATAIFA Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama amerudi katika jukwaa la kitaifa usiku wa kuamkia Jumatano ili kumuunga mkono Kamala Harris katika azma yake ya kuwania urais dhidi ya Donald Trump.
Wakiwatahadharisha Wademocrat kwamba wana mapambano makali mbele yao, rais wa zamani wa Marekani Barack Obama na mkewe Michelle, Jumanne, walitoa wito kwa Wamarekani kumkumbatia Kamala Harris katika ujumbe walioutoa katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Democratic huko Chicago.
“Marekani, matumaini yanarudi,” alisema Michelle Obama. Baada ya hapo bi Obama akamshambulia Donald Trump, kinyume na ilivyokuwa katika hotuba yake ya mkutano mkuu wa chama hicho mwaka 2016 aliposema, “wakienda chini, tunainuka.”
Credit; DW
#KonceptTvUpdates