Mwandishi Wetu,Dodoma
BENKI ya NMB imetoa mamilioni ya fedha na vifaa ikiwemo zana za kilimo, friji na TV huku ikisubiri mshindi atakayeibuka na Sh100 milioni.
Zawadi hizo zimetolewa kwa washindi kutoka mikoa mbali mbali nchini kupitia Shindano lake la Bonge la Mpango linalochezeshwa kupitia matawi yake nchi nzima.
Meneja Mauzo wa NMB Makao makuu Nehemia Simba, amesema Shindano hilo linaendelea kuwaibua washindi kwa masharti nafuu ambayo ni kufungua akaunti tu.
“Kinachofanyika ni mtu kufungua akaunti na kuweka pesa kwa kiwango kisichopungua shilingi laki moja ndipo mtu anaingia kwenye Shindano,”amesema Simba.
Meneja huyo amesema wateja wengi wananufaika kupitia mpango huo ambao hivi karibuni walitoa zawadi katika Morogoro.
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini Ibrahim Sikana amesema utaratibu wa Michezo ya Kubahatisha unaoendeshwa na benki ya NMB umekuwa wa mfano na akaomba taasisi zingine zijifunze kupitia kwao.
Sikana amesema washindi kwenye mashindano ya NMB wanapatikana kwa njia halali kwani mazingira ya Shindano ni ya wazi.
“Tunahakikisha kuwa washindi wanapatikana katika mazingira ya haki na usawa, pongezi NMB kwa sababu wanarudisha kwa jamii walichokipata kwa namna mbalimbali,” amesema Sikana.
Amesema mpango huo ndani ya NMB unahamasisha uwekezaji bora na utunzaji wa fedha jambo ambalo linapaswa kuungwa mkono.
Kwa upande wake Meneja wa NMB tawi la Udom Badie Erasto amesema Bonge la mpango limejaa zawadi mbalimbali ambazo washindi wanabeba mamilioni ya fedha.
Amesema washindi kumi kila mmoja kwenye shindano hilo wamekuwa wakishinda laki Moja kila mtu na kwamba hivi karibuni jumla ya watu 30 wameshinda laki moja na kukabidhiwa zawadi.
Kwa mujibu wa Meneja, zawadi zingine zinazotolewa kwenye shindano hilo ni TV janja, pikipiki za Toyo, Power Tiller na friji ambao wameshapokea zawadi zao.
Kwa upande wa fedha kila mwezi kila mwezi washindi wanne kila mmoja anaondoka na Shikingi wakati wakisubiri kwenye fainali ambako kitakuwa na zawadi za fedha Sh100 milioni, toyo na power tiller ambapo aliomba wananchi waendelee kuweka fedha banki.
Mwisho …..