Benki ya NMB imeingia makubaliano ya ushirikiano na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo imetenga Shilingi Bilioni Moja kwa miaka minne, ikichangia Shilingi Milioni 250 kila mwaka kusaidia matibabu ya watoto wenye maradhi ya moyo wanaopata huduma JKCI.
Makubaliano haya, yanayoanza kutekelezwa rasmi mwaka huu, yanalenga kuwezesha upatikanaji wa taarifa na huduma za afya kwa watoto wenye maradhi ya moyo na kupunguza changamoto ya gharama za matibabu kwa watoto wanaohudumiwa na taasisi hiyo, ikiwa ni sehemu ya sera yetu ya uwekezaji kwa jamii.
Mbali na mchango wa kifedha, ushirikiano huu pia unalenga:
➡️ Kushirikiana na wataalamu wa JKCI kutoa elimu ya magonjwa ya moyo kwa wafanyakazi wa Benki ya NMB, wateja, na wadau wengine ili kuongeza uelewa kuhusu afya ya moyo miongoni mwa Watanzania.
➡️ Kushiriki katika shughuli za kuchangisha fedha zaidi kwa ajili ya matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaohudumiwa JKCI.
Makubaliano haya yamesainiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa @nmbtanzania, Bi. Ruth Zaipuna, na Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dkt. Peter Kisenge, na kushuhudiwa na Afisa Mkuu wa Fedha wa JKCI, Agnes Kuhenga, na Mhazini na Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji kwa Jamii @nmbtanzania, Aziz Chacha pamoja na wafanyakazi kutoka taasisi zote mbili.
#NMBKaribuYako