Saudi Arabia inajiandaa kufungua duka lake la kwanza la pombe katika mjini Riyadh ambalo litahudumia wahamiaji wasio Waislamu pekee, ikiwa ni kwa mara ya kwanza kufanya hivyo kwa zaidi ya miaka 70.
Wateja watalazimika kujisajili kupitia programu ya simu, kupata nambari ya kibali kutoka kwa wizara ya mambo ya nje, na kuheshimu viwango vya kila mwezi vya ununuzi wao, ilisema hati hiyo, ambayo ilionekana na Reuters.
Hatua hiyo ni hatua muhimu katika juhudi za ufalme huo, zikiongozwa na Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman, kuifungua nchi hiyo ya Kiislamu yenye msimamo mkali kwa ajili ya utalii na biashara kwani unywaji pombe ni marufuku katika Uislamu.
Pia ni sehemu ya mipango pana inayojulikana kama Dira ya 2030 ya kujenga uchumi wa baada ya mafuta.
Duka hilo jipya liko katika mtaa wa Kidiplomasia wa Riyadh, kitongoji ambacho mabalozi na wanadiplomasia wanaishi, na “itazuiliwa kabisa” kwa wasio Waislamu, waraka huo ulisema.
#KonceptTvUpdates