Timu ya Taifa Tanzania “Taifa Stars” imewashukuru Watanzania kwa kuonyesha uzalendo wa kuiunga mkono katika Michuano ya AFCON 2023.
Taifa Stars imeishia hatua ya makundi baada ya kushindwa kupata pointi za kuisogeza katika hatua ya 16 bora.
“Asanteni Watanzania kwa kutuunga mkono wakati wote wa AFCON 2023 Ivory Coast, hatujafanikiwa kufuzu raundi ya 16 bora tumeumia pamoja, wakati mwingine tutarudi imara zaidi.” @TaifaStars_
#KonceptTvUpdates