Mamelodi Sundowns imethibitisha kumsajili Matías Esquivel kutoka klabu ya Argentina, Atlético Lanus kwa mkataba wa miaka minne na nusu.
Kiungo huyo anajiunga na Masandawana ikiwa ni ujio wa pili wa dirisha la katikati ya msimu, kufuatia beki Zuko Mdunyelwa aliyejiunga Desemba 2023.
Esquivel anachukuliwa na Masandawana akiwa na zaidi ya thamani ya Tzs 6.3 Bilioni kwenye soko la uhamisho wake.
Esquivel amejiunga na wachezaji wenzake wapya huko Chloorkop huku Bafana Ba Style wakirejea kutoka mapumzikoni kujiandaa na nusu ya pili ya msimu.
#KonceptTvUpdates