Katika harakati za kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja, Serikali imedhamiria kupambana na umasikini kwa kujenga Uchumi wa Kiushindani wa Viwanda. Serikali imeweka jitihada za makusudi kwa kuanzisha Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano FYDP III (2021/22 – 2025/26). Mpango huo pia unatambua umuhimu wa sekta zingine katika kuleta maendeleo kama kudumisha utawala bora, elimu, maji safi na salama, pamoja na kuunda uchumi thabiti na wa ushindani.
Kushughulikia utofauti wa mapato na matumizi katika jamii kunatambulika kama kipengele muhimu katika kufikia malengo yaliyoainishwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa. Mnamo 2023, kampuni ya Serengeti Breweries Limited iliimarisha zaidi dhamira yake ya kusaidia FYDP III(2021/22 – 2025/26).
Wakazi 2,000 wa Mkoa wa Pwani wamepata maji safi
Programu ya maji safi na salma kutoka SBL imekuwa na matokeo makubwa baada ya kujenga bwawa la usambazaji maji katika Wilaya ya Handeni, Mkoa wa Tanga, Tanzania, na kuwanufaisha zaidi ya wakazi 2,000 katika eneo la Pwani. Kwa ushirikiano na WaterAid, bwawa hilo linazalisha mita za ujazo 137,000, sawa na zaidi ya mabwawa 53 ya kuogelea ya Olimpiki. Huu ni mradi wa 25 wa SBL kutekelezwa kote Tanzania katika muongo uliopita, kutoa maji safi na salama kwa jamii za Tanzania.
Utekelezaji wa ahadi hii ya SBL inadumisha juhudi za serikali katika kuongeza usambazaji wa maji safi kwa asilimia 85 ya wananchi na asilimia 95 ya wananchi kupata huduma bora za vyoo katika maeneo ya vijijini ifikapo 2025.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Obinna Anyalebechi, alisema, “mradi huu wa maji wa TZS milioni 380 unathibitisha dhamira yetu ya usimamizi endelevu wa rasilimali za maji na unatambua umuhimu wa rasilimali hii ya thamani kwa kizazi cha sasa na kijacho”.
Usawa wa Kijinsia
Kampuni ya SBL pia kupitia rasilimali zake kwenye programu ya WASH iliundwa mahsusi kwa ajili ya wanawake wa Handeni. Mpango huu umelenga kuhakikisha ushiriki wa wanawake wa moja kwa moja katika shughuli za kila siku za mradi.
Hatua ya makusudi ya kuwawezesha wanawake katika kusimamia huduma za usambazaji maji kutoka kwenye bwawa na ushiriki katika vikao vya maamuzi ya jamii. Hii sio tu kwamba inaongeza mapato yao kwa kulipia ushuru wa maji lakini pia inawahusisha katika shughuli za kuzalisha mapato zinazozingatia mazingira, kusaidia usimamizi wa rasilimali za maji na uboreshaji wa afya kwa ujumla.
Zaidi ya hayo, programu ya WASH inaimarisha uwekaji vyoo unaofaa ambao unasaidia upatikanaji wa vifaa vya WASH kwa wasichana wakati wa vipindi vya hedhi na hivyo kuboresha mahudhurio shuleni. Kuongezeka kwa ajira na kipato:
Juhudi za serikali kuimarisha sekta binafsi imetoa mwanya kwa kampuni ya bia ya Serengeti kuzindua kampeni zinazolenga soko ili kupanua wigo wa uzalishaji, usambazaji, matumizi na ajira. Mfano mnao tarehe 21 Oktoba, SBL iliandaa moja ya matamasha makubwa zaidi Afrika Mashariki kwa uzinduzi wa Serengeti Oktoberfest, ikivutia Watanzania 5,000 na wafanyabiashara 102, mawakala, na wachuuzi mbalimbali kwenye mnyororo mzima wa
thamani na usambazaji.
SBL ilianzisha uwekezaji mwingine mkubwa wa zaidi ya TZS bilioni 2 kupitia kampeni yake ya ‘Maokoto Ndani ya Kizibo’, kwa kuwapa wateja nafasi ya kujishindia hadi TZS 500,000 kwa kila bia waliyonunua. Kampeni hiyo iliwapa wateja matarajio ya kipato cha ziada na kufungua fursa nyingi za biashara kwa wenyeji katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania, nakuingiza fedha za haraka katika uchumi.
Kuwawezesha vijana katika kilimo kwa Maisha endelevu:
Kampuni ya bia ya Serengeti ilianza safari ya kuleta mabadiliko, kushiriki kikamilifu katika mageuzi ya sekta ya kilimo kwa kukuza upatikanaji wa elimu na mafunzo bora.
Hivyo, kupitia mpango wa ufadhili wa Kilimo Viwanda wa SBL, wamesaidia zaidi ya wanafunzi 200 kutoka familia zenye kipato cha chini, wanaosoma kozi zinazohusiana na kilimo, wakilenga kuwajenga kuwa mabingwa wa mbinu endelevu za kilimo. Juhudi hizi za miaka minne zinadhihirisha dhamira ya Kampuni ya bia ya Serengeti katika kuifanya sekta ya kilimo kuwa ya kisasa nchini.
Kujenga jamii salama na unywaji wa kuwajibika
Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) inashughulikia kikamilifu suala la unywaji pombe kwa vijana wadogo kupitia Mpango wake wa ‘Smashed’, unaolenga kuwajengea uwezo vijana wenye umri mdogo wa Kitanzania katika maarifa na ujuzi wa kufanya maamuzi sahihi yanayohusu unywaji pombe.
Mpango huu unatumia sanaa za maonyesho katika kutoa elimu, kutoa jukwaa kwa wanafunzi kujadili kwa uwazi na kujifunza kuhusu madhara ya matumizi mabaya ya pombe.
Sambamba na hayo, kampuni hiyo kwa kushirikiana na jeshi la polisi ilizindua kampeni ya INAWEZEKANA ya kutoa uelewa juu ya tabia ya unywaji pombe kwa uwajibikaji, ikisisitiza unywaji wa wastani kama njia kuu ya kujikinga na majanga yatokanayo na pombe.
Mkurugenzi wa Masuala ya Ushirika wa SBL, Ndugu John Wanyancha alisema, “kampeni hiyo ni ushahidi wa kujitolea kwetu kukuza tabia za unywaji pombe kwa kuwajibika ndani ya jamii yetu ambapo tunaamini kabisa kuwa unywaji pombe unaowajibika huanza na kila mtu”.
Nishati safi na endelevu
Katika mwaka 2023, SBL pia iliendeleza nia yake ya kuunda mustakabali endelevu na wa kaboni ya chini. Kampuni inasisitiza ahadi yake ya kufikia asilimia sifuri ya kaboni katika shughuli zake zote za moja kwa moja ifikapo 2030 kwa kuimarisha juhudi zake kwa ushirikiano na washirika wa maendeleo katika kudumisha Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kupitia programu endelevu.
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba huo iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwaka jana, Mkurugenzi wa SBL, Obinna Anyalebechi, alisema: “Uendelevu ni jambo la msingi kwa biashara yetu huku tukijitahidi kuleta matokeo chanya katika maisha ya wanajamii pale tunapopata vyanzo, kuzalisha, kuishi na kuuza bidhaa mbalimbali zetu”.
#KonceptTvUpdates