Mshambuliaji wa kimataifa, Mohamed Salah analazimika kuondoka kwenye kikosi cha Misri kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika ili kuendelea na matibabu zaidi ya jeraha la misuli ya paja katika klabu yake ya Liverpool nchini Uingereza baada ya mchezo utakaochezwa leo dhidi ya Cape Verde.
Salah alipata majeraha katika mechi dhidi ya Msumbiji na anatumainiwa baada ya muda atarejea katika kikosi chake kwenye michuano hiyo inayoendelea nchini Ivory Coast.