Shirika la Reli Tanzania (TRC), limetangaza kuendelea kusitisha huduma ya usafiri wa treni kutoka Dar es Salaam kuelekea mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Katavi, Kigoma na njia ya Kaskazini kuelekea mkoani Tanga kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneo na kusababisha uharibifu wa miundombinu ya reli.
Miundombinu iliyotajwa kuharibika ni stesheni ya Morogoro na Mazimbu, Munisagara na Mzaganza wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro na Godegode na Gulwe wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma pamoja na eneo la Wami, Ruvu mkoani Pwani na Mkalamo mkoani Tanga.
Wahandisi kutoka TRC wanaendelea na matengenezo katika maeneo yaliyoathiriwa na mvua zinazoendelea.