Serikali ya Zanzibar imepiga marufuku Wamaasai kutembea na silaha za jadi mitaani kwa kile kilichosemwa na kudhaniwa kuwa ni kuhatarisha maisha ya watu na ni kinyume cha utamaduni kwa waishio visiwani humo.
Haya yanajiri kufuatia kusambaa kwa video kwenye mitandao ikiwaonyesha watu jamii ya Kimasai wakiwashambulia pembezoni mwa fukwe za bahari pia nyingine ikionyesha kumshambulia mfanyakazi wa halmashauri walipokuwa wakitekeleza operesheni ya kusimamia sheria ndogo ndogo zinazozuia kufanya biashara maeneo ya barabara ya Mji Mkongwe.
Hivyo serikali imewataka wafuate utaratibu wa kuishi kulingana na mazingira hayo na si vinginevyo.
Una maoni gani juu ya uamuzi huo uliochukuliwa na Zanzibar kwa Wamaasai?