Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, Februari 7, 2024 Jijini Dodoma amezindua rasmi kampeni ya upandaji miti katika maeneo yanayomilikiwa na Jeshi la Polisi.
Uzinduzi huo umefanyika katika kambi ya Polisi Nzuguni na baadaye viwanja vya Polisi eneo la Madenge Hill.
Zoezi hilo limeanza rasmi ili kuunga mkono jitihada za kutunza mazingira ili kuepukana na madhara yanayojitokeza kutokana na mabadiliko ya Tabianchi.
#KonceptTvUpdates