Timu ya Taifa ya Nigeria imefuzu hatua ya kucheza Fainali Michuano ya AFCON 2023 baada ya kuiondoa Afrika Kusini kwa Mikwaju ya Penati.
Nigeria iliongoza kwenye mchezo huo kwa mkwaju wa penati mnamo dakika ya 67′ kupitia nyota wake Ekong, wakati Afrika ya kusini ilijipata dakika za Mwishoni kufuatia mkwaaju wa penati baada ya Muamuzi kuona kosa Alilofanyiwa Percy Tau kwa picha za Marejeo za VAR ambapo pia ilipelekea kutohesabia bao la pili la Nigeria lililofungwa na nyota wake Victor Osmhen.
Mokoena wa Bafana Bafana alibeba jukuu la kuirejesha timu yake mchezoni, na akafanikisha kufanya hivyo ubao wa magoli ukasoma 1-1 mnamo dakika ya 90′.
Timu hizo zikaenda muta wa nyongeza pia hazikufungana hadi kutoana kwa mikwaju ya penati amabpo Nigeria 1 (4) -1 (2) Afrika Kusini.
Matokeo hayo yameifanya Nigeria kufuzu kucheza Fainali na kuiondosha Afrika Kusini kwenye michuano hiio.
#KonceptTvUpdates