Watanzania 700 wanatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa moyo kwenye kambi ya moyo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) jijini Dodoma.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa BMH, Dkt Calvin Masava, amesema hayo leo ambapo amesema kuwa BMH inashirikiana na madaktari sita kutoka Netherlands kufanya kambi hiyo ya moyo.
“Lengo la kambi mbali na kutoa huduma lakini inalenga kubadilishana uzoefu na wenzetu kutoka Netherlands,” ameeleza Dkt. Masava Dkt . Masava amefafanua kuwa watakaokutwa na matatizo ya moyo watapatiwa matibabu hapa hapa BMH. Hata hivyo amesema kuwa hiyo ni kambi yao ya kwanza ya pamoja na wenzao kutoka nje kwa mwaka huu.
#KonceptTvUpdates