Mahakama ya Wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma imemuhukumu mshitakiwa Moses Method(23),mkulima,mkazi wa Kijiji cha Kasuga wilayani Kakonko kwenda jela maisha na kulipa fidia kwa muhanga ya fedha taslimu Tsh.1,000,000 baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili(9).
Mshitakiwa alitenda kosa hilo Agisti 17,2023 huko Kijiji cha Kasuga Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma.
Mshitakiwa alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Agosti 21,2023.
Akitoa hukumu hiyo Februari 12,2024 hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Kakonko mheshimiwa Ambilikile Kyamba amesema kuwa Mahakama imejiridhisha pasipo na shaka ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka na hatimaye kumtia hatiani mshitakiwa kwa kosa hilo.
Mshitakiwa huyo amehukumiwa kifungo hicho ili iwe fundisho kwa wahalifu wanao jihusisha na vitendo vya ukiukaji wa sheria,maadili na ukatili dhidi ya watoto.
#KonceptTvUpdates