Kupitia ukurasa wake binafsi wa mtandao wa kijamii wa ‘X’ zamani ikijulikana kama ‘Tweeter’ Waziri Nape Nnauye ametolea ufafanuzi kwa kuweka chapisho kufuatia katazo la kutumia mbwembwe wakati wa kusoma magazeti na kuruhusu ubunifu huo (vionjo) uendelezwe na wanahabari.
“Nimeona mjadala wa ‘kusoma magazeti’, nimeelekeza TCRA kuruhusu ubunifu kwenye tasnia ya Habari, staili ya usomaji wa magazeti imeongeza mvuto kwenye usomaji huo, ni jambo linalopaswa kutiwa moyo badala ya kuzuiwa, Waandishi endeleeni na ubunifu kwenye kusoma magazeti” -Nape
“Maelekezo mengine yoyote ambayo TCRA inatoa kwenye sekta ya habari yanapaswa kuwa wezeshi na sio zuizi, ni muhimu TCRA ijenge utamaduni wa kuzungumza kabla ya kuagiza” -Nape
Tukirejerea katika mkutano wa mwaka wa watoa huduma wa sekta ya utangazaji (Annual Broadcaster’s Conference -ABC) uliofanyika kwa siku mbili kuanzia Februari 13 hadi 14 mwaka huu, jijini Dodoma, mkutano ambao mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Methew, Meneja wa kitengo cha utangazaji TCRA Mhandisi Andrew Kisaka alitoa tamko la kupiga marufuku usomaji magazeti kwa ‘mbwembwe”.
#KonceptTvUpdates