WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa afungua Mkutano wa ‘FUTURE READY SUMMIT’ Uliowakutanisha Wadau, Wafanyabiashara, Waanzilishi wa Kampuni Chipukizi za Ubunifu wa Kidigitali Nchini, Februari 15, 2024 Jijini Dar Es Salaam.
Picha: Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa (wa pili kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Ulinzi wa Mtandao wa Vodacom Tanzania, Macbethana Wilfred kuhusu jitihada za kampuni hiyo kukabiliana na matukio ya uhalifu wa kimtandao wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Future Ready Summit uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wakimsikiliza wa kwanza kushoto ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mh. Nape Nnauye na kutoka kulia ni Mkurugunzi wa Vodacom Tanzania, Philip Besiimire akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hiyo, Jaji Mstaafu Thomas B Mihayo.
Picha: Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa (wa pili kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Upelelezi wa Mtandao wa Vodacom Tanzania, Joseph Mnyune kuhusu jitihada za kampuni kukabiliana na matukio ya uhalifu wa kimtandao wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Future Ready Summit uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wakisimkiliza wa kwanza kushoto ni Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mh. Nape Nnauye na kutoka kulia ni Mkurugunzi wa Vodacom Tanzania, Philip Besiimire akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hiyo, Jaji Mstaafu Thomas B Mihayo.
Picha: Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa (wa pili kulia) akitazama namna utoaji wa mafunzo ya teknolojia na masomo ya sayansi kwa wanafunzi wa kike kupitia programu ya ‘Code Like a Girl’ inayoendeshwa na Vodacom Tanzania nchini. Akishuhudia tukio hilo ambalo liliambatana na ufunguzi wa mkutano wa Future Ready Summit uliofanyika jijini Dar es Salaam leo, ni Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mh. Nape Nnauye.
Maonyesho haya yanawalenga wabunifu na wafanyabiashara wachanga ambao wanatafuta majukwaa ya kuonyesha ubunifu wao na kukutana na wadau wanaoweza kuwekeza kwa mitaji kwenye biashara zao.
Pia, ni sehemu nzuri kwa wadau wakubwa wa masuala ya kiteknolojia wanaotafuta ubunifu mpya kwenye sekta ya teknolojia wakiwa na shauku ya kukutana na wenzao.
Kwa kuongezea, bila shaka kuna wafanyabiashara na wadau tofauti ambao wanapenda kuwekeza, kutumia teknolojia katika biashara au huduma zao, pamoja na kuchangia maendeleo ya jitihada hizi, basi hii litakuwa tukio sahihi kwa wao kuhudhuria.
Hiyo ni kwa ufupi kuhusu FUTURE READY SUMIIT
#KonceptTvUpdates