Mkurugenzi Mtendaji wa Shule Direct, Faraja K. Nyalandu akizungumza na vyombo mara baada ya mara baada ya uzinduzi wa jukwaa la kielimu la SMS Makini ambalo litakuwa linatoa masuala mbalimbali ya kijifunza kupitia mtandao kwa walimu na wanafunzi wa shule za sekondari nchini mapema mwishoni mwa wiki iliyopita ,Hafla ya uzinduzi ilifanyika katika shule ya sekondari Azania Jijini Dar es salaam. |
Wanafunzi wa shule ya sekondari
Azania ya jijini Dar es Salaam wakielekezana namna ya kutumia jukwaa la kielimu la SMS Makini ambalo litakuwa linatoa masuala mbalimbali ya kijifunza kupitia mtandao kwa walimu na wanafunzi wa shule za sekondari nchini mapema mwishoni mwa wiki iliyopita ,Hafla ya uzinduzi ilifanyika katika shule ya sekondari Azania Jijini Dar es salaam. |
Kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania kwa kushirikiana na asasi ya ndani inayofanya ujasiriamali kwa njia ya mtandao, Shule Direct imezindua jukwaa la kielimu la SMS Makini ambalo litakuwa linatoa masuala mbalimbali ya kijifunza kupitia mtandao kwa walimu na wanafunzi wa shule za sekondari nchini.
Meneja wa Huduma za jamii wa Tigo , Woinde Shishael alisema wakati wa hafla ya uzinduzi huo kwenye Shule ya Sekondari Azania jijini Dar es Salaam leo kwamba SMS Makini zitawawezesha wanafunzi kuzifikia zana za kujifunza kidijitali kupitia mtandao na hivyo kuziba pengo lililopo la rasilimali za kujifunzia kwenye sekta ya elimu.
“Kupitia matumizi ya SMS Makini watumiaji wa Tigo, na hususan wanafunzi na walimu wa shule za sekondari wataweza kuipata miuhtasari ya kidijitali, mafunzo, mazoezi, kupata maelezo pamoja na video moja kwa moja kupitia simu ya mkononi,” alisema Woinde.
Alieleza kwamba madarasa yatakayohusishwa kwenye jukwaa hilo ni kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne na kuongeza kuwa maelezo ya mafunzo yatakuwa yanazingatia mtaala wa elimu wa Tanzania ukihusisha masomo tisa.
Masomo hayo ni pamoja na Historia, Uraia, Jiografia. Fizikia, Kemia, Kiingereza, Hisabati na Kiswahili.
Kwa mujibu wa Woinde SMS Makini za Tigo pia zitawaunganisha walimu na wanafunzi na fursa ya kujadiliana, kushirikishana mawazo, kurejea, na kupakua mitihani iliyopita ya Baraza la Mitihani la Taifa na hali kadhalika kuwasiliana kwenye mtandao na wanafunzi 10,000 waliosajiliwa.
Wateja wa Tigo wataweza kuipata huduma hiyo bure kwa mwezi mmoja na baada ya hapo watakuwa wanatozwa ada ya siku ya shilingi 100 na ada ya wiki ya shilingi 500, alisema Woinde.
Kuipata huduma hiyo wateja wa Tigo wanatakiwa kutuma neno ‘Makini’ kwenda namba 15397 na baadaye kufuata maelekezo yatakayokuwa yanatolewa.
Ushirikiano na asasi ya Shule Direct ni sehemu ya mkakati wa Tigo wa kuunga mkono miradi ambayo ina manufaa makubwa ndani ya jamii.
– mwisho –