Kijana aliye-trend sana Mitandaoni kupitia Mahusiano na Zari Hassan “Zari The Bosslady”, Shakib Cham amefuta picha zote zakiwa na mrembo huyo na kuonyesha kuwa kama amejutia uamuzi wa kuwa nae kwenye mahusiano ya kimapenzi huku akiacha ujumbe mzito Instagram
Shakib ameandika “May People with pure intentions find people with pure intentions.. 🙏” akimaanisha Waache watu wenye dhamira za kweli watafute wenza wao”. Kutokana na Video aliyopakia mtandaoni msanii Diamond Platnumz akiwa na Zari wakitembea huku wimbo wa “Mapoz” ukichezwa kama “Background”, imewapa neno mashabiki na wadau wa “Couple” hiyo kuhusianisha na tukio hilo kuwa huenda amefuta picha hizo watakuwa wameachana hivyo mrembo huyo amerudiana na Diamond tena.
Wadau wengine wamehisi kama ni kiki ya kuteka Mashabiki katika harakati za ku-promote wimbo huo.
Je una maoni gani kuhusu mtazamo wa mashabiki kuwa ni “KIKI”?
Dondosha Comment yako hapa!
#KonceptTvUpdates