“Tumieni vizuri taaluma mnayo patiwa na walimu ili muweze kujiajiri na kuepuka dhana ya kusubiri ajira za mitaani”
Kauli hiyo imetolewa Machi 07, 2024 na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi kutoka Dawati La Jinsi na Watoto mkoa Wa Dodoma Michael Sabuni wakati akizungumza na wanafunzi wa chuo cha ufundi stadi veta Dodoma.
Sabuni amewaasa wanafunzi hao kuto kubweteka na taaluma wanayopewa na kuendana na kasi ya mabadiliko ya kiuchumi na kujiajiri ili kuleta maendeleo ya taifa na kuachana na makundi ya uhalifu.
Aidha, Mkaguzi wa Polisi Theresia mdendemi alisisitiza utoaji wa taarifa za ukatili kwa Jeshi la Polisi pindi wanapoona ugumu wa kufikisha taarifa hizo basi wafikishe kwa walezi wa wanafunzi Matron /Patron.
#KonceptTvUpdates