Mahakama maalum inayosikiliza makosa ya udhalilishaji Mkoa wa Kaskazini Pemba imemhukumu kutumikia chuo cha mafunzo (jela)kwa muda wa miaka 70 kijana Mohammed Shaaban Said (20) mkaazi wa kijiji cha Chamboni, shehia ya Micheweni, Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba baada ya kupatikana na hatia ya makosa matano kati ya sita yaliyokuwa yanamkabili ambayo ni kubaka, kuingilia kinyume na maumbile na kutorosha msichana.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashitaka wa serikali kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa mashitaka (DPP) Zanzibar, Juma Ali, kuwa kijana Mohammed alituhumiwa kutenda makosa 6 ambayo mawili ni kutorosha msichana kinyume na kifungu 113(1)(a), makosa mawili ya kuingilia kinyume na maumbile kinyume na kifungu 133(a) na makosa mengine mawili ya kubaka kinyume na kifungu cha 108(1)(2)(e) na 109(1) vifungu vyote vya sheria ya jinai namba 6 ya mwaka 2018 sheria ya Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, makosa ambayo aliyafanya siku na eneo moja kwa watoto wawili wa kike mmoja mwenye umri wa miaka 10 na mwingine mwenye umri wa miaka 15.
Aliongeza kwamba Juni 16,2023 majira kati ya saa 4:00 za asubuhi na saa 4:20 asubuhi huko katika kijiji cha Kichange, Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba bila ya halali na bila ya ridhaa ya wazazi wake alimtorosha msichana mwenye umri wa miaka 10, kisha kumuingilia kinyume na maumbile na baadae kumbaka ambapo katika tukio hilo alishitakiwa kwa makosa matatu ikiwa ni pamoja na la kutorosha, kuingilia kinyume na maumbile pamoja na kubaka.
Sambamba na tukio hilo mtuhumiwa pia alishitakiwa kwa makosa mengine matatu ambayo ni kutorosha msichana, kuingilia kinyume na maumbile pamoja na kubaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 15 ambapo tukio hilo alikifanya Juni 16 mwaka 2023 majira ya saa 4:20 za asubuhi kwa kuwachukua watoto hao kutoka eneo la Kichange ambalo walienda kuokota mwani kuwapeleka katika eneo mbalo ni la msitu na kuanza kuwaingilia kwa zamu huku akiwa ameshika kisu mkononi kwa kuwatishia kuwa atakayepiga kelele atamuua.
Jumla ya mashahidi 7 walifika na kutoa ushahidi wao akiwemo Sajenti wa Polisi Asya Soud kutoka Dawati
#KonceptTvUpdates