Jeshi la Polisi kikosi cha kuzuia Wizi wa Mifugo STPU Kimesema Kinawashikilia watuhumiwa kadhaa kwa tuhuma za wizi wa mifugo na utoroshaji Mifugo nje ya nchi huku likisema kuwa litaendelea kushirikiana na wananchi kwa karibu ili kudhibiti uhalifu huo hapa nchini.
Akitoa taarifa hiyo Machi 12,2024 kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo Nchini Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Simon Pasua wakati alipotembelea mnada wa Tinde uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mkoani Shinyanga amesema Jeshi hilo linawashirikilia watuhumiwa wa wizi wa mifugo katika maeneo tofauti tofauti hapa nchini.
Kamanda Pasua ameongeza kuwa watuhumiwa waliokamatwa kwa tuhuma za wizi wa mifugo katika maeneo tofauti hapa nchini majina yao yamehifadhiwa